PENZI TAMU[III]
Dongobesh walikuwa wanacheza mechi ya mwisho dhidi ya timu ya Madunga ambayo ilikuwa ni mpinzani wa jadi. Sospeter kwa kuitikia mwito wa rafiki zake waliokuwa wanamsifia Suma aliamua kwenda kuangalia mechi hiyo, siyo kwa ajili ya kuona nani atashinda bali kuona kama kweli hizo sifa za Suma zilikuwa ni za kweli au ni porojo tu za kwenye Umiseta. Alipofika na kumuona jinsi binti huyo alivyokuwa anapendeza katika mavazi yake ya netiboli ambayo yalimfanya aonekana kama amepotea toka Mbinguni na wanamtafuta, Sosi alijikuta akimkodolea macho dada wa watu utadhani ameona hazina ya mfalme Solomoni. Sosi hakutaka kuangalia kitu kingine chochote na alijikuta anaungana na wadau wengine kushangilia kila Suma alipokuwa akitoa pasi na kudaka mpira. Mara mbili alijikuta anagonganisha macho yake na Suma ambaye na yeye alianza kumwangalia na kila akidaka mpira basi anaweka madoido kidogo kumlingishia Sosi (kama ilikuwa kweli au hayo ni mawazo ya Sosi tu miye sijui).
Mechi iliisha kwa timu ya Dongobesh kushinda na furaha kubwa ilitawala upande wa mashabiki wa Dongobesh wakiongozwa na shabiki aliyejipachika Sospeter Mkiru. Ilikuwa ni furaha kubwa kwani timu ya Dongobesh haijawahi kuifunga Madunga kwa miaka mitano mfululizo hivyo ilikuwa ni furaha kwa mwalimu wa Michezo Michael Tluway wa shule hiyo. Aliyekuwa na furaha zaidi ya Sosi alikuwa ni matroni wao Vera Akonaay. Wakiwa katika shamrashamra za kusherehekea Sospeter alitembelea kumwelekea Suma aliposimama mbele yake alijikuta ananyosha mkono wa pongezi kwa kapteni huyo wa Dongobesh.
“Hongera Sana kapteni” alisema Sosi huku moyo ukimwenda kasi utadhani aliyefukuzwa na simba mwenye njaa.
“Asante sana” Alijibu Suma huku akijaribu kuachilia mkono wa Sosi ambaye alikuwa kama amemng’ang’ania.
“Umecheza vizuri kweli” alijikuta akisema maneno yasiyo na kichwa wala mguu.
“Ndiyo, ila kulikuwa na mtu ananikodolea macho utadhani amepoteza kitu na mimi nimemfichia” Alisema Suma huku mikono yake akiifunga pamoja kifuani. Sosi alishindwa kujizuia kuangalia kifua cha Suma ambacho kilikuwa kimetuna kwa matiti yaliyolala kama paa nyikani na kama midomo ya hua wawili chuchu zake zilionekana kwa mbali. Sosi alimeza fundo la mate kwa aibu.
“Wala usisema maana nilichopoteza nimekipata” Alisema huku akijikaza. Waliweza kuona macho ya watu yakiwaangalia imekuwaje watu hao wawili wazungumze. Na vijana wengi walishangazwa ni jinsi gani Sosi alikuwa na ujasiri wa kuzungumza na binti mrembo kama huyo. Wengine walikiri kuwa kama kulikuwa na mwanafunzi yoyote kwenye mashindano hayo ambaye angeweza kumsimamisha Suma basi alikuwa ni Sospeter.
“Umekipata? Na ulipoteza nini?” alihoji Suma huku macho yake yakimganda kijana wa watu. Moyoni alijisemea kuwa alikuwa ni kijana mzuri, msafi, na jasiri maana vijana wengi walikuwa wanaogopa hata kumsalimia. Walijiona hawafai mbele zake.
“Nimepoteza akili yangu baada ya kukuona, na nadhani nimepata mke kwa maisha yangu yote” Kama mtu aliyepagawa pepo wa mahaba Sosi hakujua maneno hayo yametoka wapi, maana yalibubujika kama chemchemi ifukayo maji ya mapenzi.
“Wacha we!, yaani kuniona tu umeona na mke kabisa!?” Aling’aka Suma huku akikunja uso wake kwa kushangaa na kwa kukutwa hakujiandaa kwa maneno hayo. “Usiniambie umeshaona na watoto na wajukuu?” Aliendelea huku akiangua kicheko.
“Tena watatu, wawili mapacha” Alisema Sosi huku akihesabu kwa vidole vitatu kwanza, kisha viwili. Suma aliendelea kucheka huku akishikilia mbavu zake kwani hajawahi kukutana na mvulana aliyejua anachotaka kama huyo. Mara mmoja wa wanatimu wa Suma walimuita ili waende kubadili nguo na kujiandaa kwa chakula cha jioni.

Comments
Post a Comment