MAMA VANESSA SEHEMU YA 16.

Walishangaa sana maana hawakutarajia kumkuta binti huyo kwenye hiyo nyumba. Kwanza Kimaro alikuwa akijua kuwa binti huyo alikuwa akikaa na pacha wake. Walianza kusalimiana huku kila mmoja akionesha ni jinsi gani ameshtushwa. Wakati wakiendelea kusalimia kuna mwanaume aliingia ghafla.

“Vipi mke wangu, naona umepata ugeni?”

“Ndio mme wangu naona wakejuka na dalali ingawa huyu mmoja ni shemeji yangu mchumba wake na Julieth”

“Aisee karibuni sana vyumba hapa vipo kwenye hali nzuri”

“Sawa tunaomba tuvione”.

Juliana aliacha kufua na kuingia ndani kuchukua funguo. Alitoka na kuwakabidhi. Kutokana na mazunguzo hayo ni dhairi kuwa huyo ndio alikuwa mchumba wa Juliana. Kila mtu alikuwa na maswali mengi kichwani lakini waliachana nayo na kuangalia chumba. Chumba kilikuwa kizuri sana na hata Lucas alikipenda lakini swali je ataweza kuishi karibu na Juliana hili hali binti huyo walishawahi kushiriki tendo la ndoa. Walipelekwa sehemu mbali mbali lakini bado nyumba hizi hazikuwa kwenye hali nzuri kama ile ya mwanzo.

“Kaka nyie ni watu wenye hadhi yenu kuliko kuangaika mimi nashauri mchukue chumba kule pa kwanza” Dalali alipendekeza.

“Ujue mimi napenda kukaa nyumba ambayo baba au mama mwenye nyumba hakai hapo”Lucas alionesha wasiwasi.

“Ile haina shida kabisa yule aliyeingia japo ni kijana mdogo ndo mwenye nyumba. Yule hakai pale kabisa yeye ana nyumba yake na familia yake. Yule dada ni mchepuko wake tu ndo amempa chumba kimoja. Siunajua mambo ya mjini. Lakini Yule ni mfanyabiashara na wala hata hakai sana Tanzania muda mwingi yupo Kenya.”

Ufafanuzi huo kidogo ulimwingia Kimaro amabye hofu yake ilikuwa je Kimaro ataishi vipi nyumba moja na Juliana hili hali tayari yeye ana mipango yake na mama Vanesa.

“Basi tutakutafuta baadaye tulipe na upate chako” Kimaro aliongea na kumruhsu dalali aaendelee na shughuli zake. Hakumuacha hivi hivi alitoa noti ya elfu 10 na kumkabidhi. Kimaro na Lucas waliondoka na kwenda mahali ili waweze kuchambua kama wachukue kile chumba ua la.

Kimaro alaimshauri Lucas kuwa wachukue tu hasiwe na hofu na hayo mambo mengine yatajiseti tu yenyewe. Lucas alimwelezea hofu yake maana wanawake wanakuwa na wivu sana. Ilibidi Kimaro anyanyue simu na kumpigia Julaina shemu wake na kumuuliza kama yule ni mme wake. Juliana alaikiri hilo na kusema amekuwa naye kwa sababu za kimaslai na anajua kama ana mke na watoto. Juliana alitumia nafasi hiyo kumuuliza kwa nini walikuwa wakitafuta chumba? Kimaro ilibidi amdanganye kuwa kuna mtu alikuwa akitaka kuamia hapo. Basi Kimaro kwa kuyapima maneno ya huyo binti aliona kuwa hapo pata leta shida maana binti uyo na yeye alikuwa amemepnda sana Lucas.

“Mpango upo hivi ile room tusichukue badala yake tuendelee kutafuta taratibu. Naamini tutapata.”Kimaro alipendekeza. Lucas alitingisha kichwa kukubaliana na ukweli huo. Maana hata yeye alijua ni jinsi gani itamwia ngumu kutimiza malengo yake. Mara simu ya Kimro iliit ana kuangali alikuwa ni yule dalali. Dalali kwa mbwemmbe alimwambia amepeta chumba kizuri zaidi yaani hicho hakina haja ya kujifikiria mara mbili mbli kinafaa kabisa. Basi iliwalazimu kwenda kukiangalia. Kweli walijirizisha kuwa kilikuwa kinakidhi vigezo vyao. Walilipa na sasa Lucas alikuwa tayari kwa kuamia.Ilimlazimu Lucas kurudi Musoma ambapo sasa alirudi ili kuweka mambo sawa ikiwa ni pamoja na kuchukua vitu vyake.

Kwa msaada wa rafiki yake huyo aliweza kupata gari ambalo lilikuwa linaenda Mwanza. Aliamisha vitu vayke vyote akawa amehama rasmi Musoma. Alimweleza mama Vanesaa ambaye na yeye alioneshwa kufurahishwa sana na kilichojiri hivyo na alimtuma fedha zingine ili aweze kufanikisha jambo hilo kwa urahisi. Kweli maisha yanabadilika na sasa Lucas alikuwa hawezi tena kazi ambayo alikuwa amefukuzwa. Wala alikuwa hawazi tena kuhusu mkewe zaidi ni kulipa kisasi. Aliendelea na maisha na wala hakuwa na hofu yoyote. Kila siku alikuwa akiwasiliana na mama Vanessa na mwanamke huyo aliendelea kumsihi kuwa hasiwe na wasiwasi kwa sababu yeye yupo na atamsapoti kwa hali na mali. Maisha yakasonga na mama Vanessa alimwibia pesa mume wake na kumkabidhi bwana Lucas. Lucas hakuamini macho yake maana alipewa fedha na pia alipewa chaneli za kufungua biashara ambayo itamnufaisha kwa muda mfupi.

Mambo yalipoanza kuchanganya ndipo kule kazini walimpigia simu na kumwambia kuwa boss ameamua kumsamehe na anatakiwa kurudi kazini. Boss wake alipata tabu sana na ilimuumiza kisaikolojia maana pamoja na ubaya wote aliomfanyia lakini Lucas hakuenda hata idara ya kazi. Wala hakuwahi kumsumbua na wala hakuwahi kumtafuta mke wake. Kuna roho ya ubinadamu ilimrudia na kuona kuwa ipo haja ya kumpumbaza tean bwana Lucas. Lucas alifikiria sana kwa nini boss wake anataka kumrudisha kazini. Alijiuliza au amegundu akuwa ana uhusano wa siri kwa siri. Ilibidi jambo hilo amshirikishe bwana Kimaro na kuona atamshauri nini. Bwana Kimaro alicheka sana na alimwambia kuwa huo ni mtego hivyo kamwe hasirudi nyuma. Kimaro alimwambia kuwa huenda boss wake ameshagundua kuwa anatoka na mke wake hivyo ikawa njia moja ya kutaka kummaliza kabisa.

Lucas akaona haitoshi ikamlazimu kumpigia mama Vanessa na kumuomba ushauri juu ya yeye kurudishwa kazini. Mama Vanesaa alimuuliza maswali magumu kabla ya ya kumshauri. Kwanza alimuuliza huo mshahara ulikuwa ukimwingizia shilingi nagapi na hiyo biashara anayofanya sasa hivi inamwingizia shilingi ngapi na kama akiongeza juhudi itamwingizia shillingi ngapi. Mama Vanesa akamwambia wikiend hiyo aende Mwanza ili waweze kujadili jambo hilo kwa umakini lakini kwa kifupi hasirudi nyuma kamwe. Wakati akiongea na mama Vaness kuna simu ilikuwa ikipiga kwenye simu yake. Alipokata alikuta missed call ya Mishel mke wake wa ndoa. Hajakaa sawa mkewe alikuwa akipiga tena simu na kumfanya akunje uso kwa hasira…****ITAENDELEA*******

Comments

Popular posts from this blog

Vifahamu Vitu Vidogo Vidogo Ambavyo Huzidisha Utamu wa Mahusiano Katika Mapenzi

UTAMU WA MCHEZO SEHEMU YA 2

Jinsi ya kumtoa msichana Bikra bila maumivu, wengi hawajui hili, Cheki hapa.