PENZI TAMU[II]

Ilikuwa mwaka 1992 kwenye mashindano ya Umoja wa Michezo ya Sekondari Tanzania ngazi ya Mkoa ambayo kwa mara ya kwanza yalikuwa yanafanyika kwenye shule ya Sekondari ya Karatu iliyopo pembezoni mwa barabara iendayo mbuga maarufu ya Serengeti nje kidogo tu ya mji wa Karatu. Wakati huo mji wa Karatu ulikuwa bado ni Wilaya ndogo katika mkoa wa Arusha. Shule karibu ishirini za Sekondari kutoka kila kona za mkoa wa Arusha zilikuwa zinawakilishwa kwenye mashindano hayo ambayo hatimaye yangeteua timu ya mkoa ambayo ingewakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano ya UMISETA yaliyokuwa yanafanyika baadaye mwaka huo huko Morogoro. Sospeter alikuwa ni golikipa namba moja wa timu ya Soka toka shule ya sekondari ya Singe iliyoko Babati. Sifa zake zilienea kwenye mashindano hayo kwani aliokoa penati tano katika mechi mbalimbali ambazo ziliifanya timu yake kushiriki katika mashindano hayo. Hata hivyo sifa hizo hazikumfanya awe anajipendekeza au kujiona yeye bora zaidi. Nje ya uwanja alikuwa ni kijana mcheshi, mwenye kupenda utani, lakini anayeheshimu kila mtu. Akiwa kwenye lango alikuwa ni tishio kwa timu ya ugeni kwani alikuwa na manjonjo ya Juma Pondamali na udhibiti wa goli wa Idi Pazi. Alikuwa na mbwembwe golini kiasi cha kuwafanya washambuliaji wa timu ya ugeni kupenda kujaribu mashuti ya mbali kwani wakimsogelea huwa anawazogoa na kuwatania kiasi cha kuwafanya wakasirike na hivyo kushindwa kutilia mkazo ufungaji magoli. Kwa mtindo wake huo watu walimfananisha na aliyewahi kuwa golikipa wa Coastal Union, Duncan Mwamba.

Upande mwingine kulikuwa na timu ya Netiboli toka shule ya Sekondari ya Kilutheri ya Dongobesh wilayani Mbulu. Kati ya shule zote zilizowakilishwa kwenye mashindano hayo timu ya Dongobesh ndiyo ilionekana kutoka mbali zaidi na wachezaji wake kuonekana ndio washamba zaidi. Hata hivyo watoto wengi wa wakubwa ambao walikuwa watundu huko mijini walitupwa huko kwenye shule hiyo ya bweni iliyozungukwa na kijiji cha kale cha Dongobesh. Timu yao ya Netiboli ilikuwa inacheza vizuri lakini sifa kubwa ilikuwa inatokana na dada aliyekuwa akicheza nafasi ya senta, alikuwa ni gumzo hapo Karatu. Kwanza kwa sababu ya uzuri wake na umbo lake la kimalaika. Wenyewe walimpachika jina la Angel hadi wengine walidhania ndio jina lake halisi. Alikuwa na mvuto wa ajabu kwa wavulana na wasichana. Lakini pamoja na sifa zake zote Suma alikuwa anaakili darasani na tangu aingie shule ya Dongobesh hajawahi kushika nafasi chini ya pili. Alikuwa akipishana na kijana mmoja ambaye baadaye alijulikana kwa kazi yake ya uandishi, hadithi, na utunzi mbalimbali kwenye mtandao wa kiintaneti.

Comments

Popular posts from this blog

Vifahamu Vitu Vidogo Vidogo Ambavyo Huzidisha Utamu wa Mahusiano Katika Mapenzi

UTAMU WA MCHEZO SEHEMU YA 2

Jinsi ya kumtoa msichana Bikra bila maumivu, wengi hawajui hili, Cheki hapa.