MAMA VANESSA MWISHO SEHEMU YA 20

Yule daktari kwa kuwa alikuwa akimjua aliamua kulivaa swala hilo na kumsaidia. Alimweleza kuwa hasiwe na hofu yeye ataandika ripoti itakayo msaidia lakini pia kwa sasa wasiseme kua amefariki ili kama kuna mali anaweza kuamisha afanye hivyo maana akisubiri mgao wa halali ndugu wanaweza kumdhulumu. Kidogo mama Vanesa akawa amepata nafuu na kuona kumbe anaweza kukwepa mkono wa sheria. Daktara alimwambia habari za kifo zitatangazwa kesho. Mama Vanesaa aliondoka na kuelekea nyumbani. Yaani akili yake ilikuwa imechanganyikiwa kwa kiwango kikumbwa. Alifika akafungua kabati ambalo huwa linawekwa pesa. Baba Vanesaa ni miongoni mwa watu ambao huwa wanahifadhi kiwango kikumbwa cha fedha tena dola za Kimarekani. Ilikuwa ni fursa nzuri kwake maana alizijaza kwenye begi kasha kwa haraka alitoka nje.

Alifanya kwa haraka na kuziweka kwenye gari lake binafsi. Lengo ni walinzi wasijue kama ameondoka na mizigo hakuhitaji dereva aliwasha gari na kuondoka. Aliwaza pa kuzipeleka hizo fedha akaona njia pekee ni kuzipeleka kwa Lucas. Huyo alinyoosha barabra ya Mwanza. Alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi sana. Ndani ya masaa mawili alikuwa jiji la Mwanza. Moja kwa moja alienda mpaka mataa ambao Lucas alikuwa amepanga. Alipiga honi lakini geti alikufunguliwa kwa haraka. Aliamua kuingia mwenyewe nia ni kumpa hizo fedha Lucas na yeye arudi zake Musoma tayari kukamilisha janga lilokuwa mbele yake. Alipiga hatua kuuelekea mlango wa Lucas. Mlangoni tu alikaribishwa na viatu vya kike lakini hakujali. Aliugusa mlango na kwa bahati nzuri ulikuwa wazi.

“Hodi humu ndani” alibisha na kuingia moja kwa moja. Palikuwa kimya na maji yalikuwa yakimwagika bafuni.Ishara kuwa kulikua kuna mtu anaogoa.Muda huo Lucas na Juliana walikuwa wameshamaliza raundi ya asubuhi na kuamua kujisafisha kabla ya kwenda kupata kifungua kinywa.

Lucas alibahatika kuiskia hiyo sauti na pia aligundua kuwa alikuwa n mama Vanessa. “Shiiiiiiiiiiiii iiiiiiiii” alimwekea ishara ya kidole Juliana akaimtaka atulie maana tayari wameshafumaniwa. Akamsogelea na kumwambia yeye anatoka kisha yeye abaki humo na afunge kwa ndani. Juliana alitingisha kichwa ishara kuwa ameelewa. Lucas akiwa uchi alitoka bafuni.

“Jamani mama Vanesaa mbona umekuja kwa kunisthukiza kuna usalama kweli”

“Usalama hakuna maana mlangoni nimeona viatu vya kike na pia hapa kitandani nimeona nguo za kike. Lucas ina maana mimi sikuridhishi mpenzi, mbona nimejitolea kila kitu kwako kwa nini wanaifanyia hivi?”Mama Vanesaa aliongea kwa sauti ya upole mmno.

“Hakuna chochote mama Vanesaa hizi nguo na vile viatu ni vya mke wangu.Huwa nikimiss natoa nguo zake kwenye begi naziangalia. Na vile viatu niliviweka atleast majirani wajue kuwa na mimi nina mwanamke. Nimefanya hivyo maana kuna dada hapo alikuwa akijipendekeza pendekeza kushinda vishawishi nimemuweka yeye akiona najua wewe upo” Lucas aliongea uwongo unaofanaa na ukweli

“Ooooooops!!!!!! Tambua nakupenda sitaki kukuchunga japo wadanyanya ila iwe mwanzo na mwisho kuingiza wanawake kwenye hii nyumba. Jiheshimu utafaidi vingi kutoka kwangu.”

“Nimekuelewa mama Vaenesa, nami nitakupenda daima.

“Lucas wewe kwa sasa ndo utakuwa mme wangu maana Baba Vanesaa amefariki dunia..

“Amefarik dunia kwa sababu gani!!!!!!!!!!!”

“Pombe, amekunywa pombe nyingi sana na alivyokuja nyumbani amejigonga kwenye ukuta ndo umauati umemtwaa.

“Bado ni siri ila nimekwambia wewe tu ili ujue hilo..

‘Sasa hiyo si ni kesi kwako”

“Mimi sio pombe hakuna kesi..

“Aisee Mungu ni mwema, aende salama na malipo ni hapa hapa duniani..Leo huenda nikafanya sherehe kumbwa sana.

“Kuwa na utu usishabikie kifo..Kwanza haya siyo yaliyonileta hapa ebu njoo nifuate.”Mama Vanesa aliongea na kuanza kuondoka. Lucas na yeye alianza kumfuata kwa nyuma. Alivyotaka kutoka akagundua kuwa alikuwa uchi. Alirudi na kuvaa nguo. Mama Vanesa na yeye alirudi na kumwambia “Inelekea hizi nguo ndo zinakuchangnya ngoja niende nazo” Akanyanyua zile nguo za kike akatoka nazo. Alivyofika mlangoni akachukua na viatu kisha akaenda navyo kuvifungia kwenye buti la gari. Ni kama vile aligundua humo ndani kulikuwa na mwanamke hivyo aliamua kumkomesha.

“Nisikileze kwa umakini. Matatizo haya yalionikuta ni makubwa. Kwa kuwa naweza hata ingia gerezani kwa hatia yakupasa mimi na wewe tuwe kitu kimoja. Nihadi kuwa utakuwa nami

“Nitakuwa na wewe usijali.

“Yakupasa upambane kwa hali na mali kunilinda..Hili begi lina pesa nyingi sana ambazo zinatosha kutufanya tuishi masha ya raha baada ya msiba. Nakukabidhi uzihifadhi sehemu salama na tutaanza maisha mimi na wewe.Usiangalie nyuma kwamwe na kamwe usinisaliti. Achana na habari za tama na wanawake watakuibia na kukufilisi..

“Nimekuelewa mama Vanesa na kwa hili ondoa shaka nitakupenda daima.

“Mkeo hakuwa mwaminifu usifikirie kumrudia maana kama sasa ukimsamehe na mbeleni anaweza kuja kukusaliti tena kwa sabab ya pesa.Nisikuchoshe nenda kamtoe na huyo kahaba huko ndani mwambie akome au atafute vya kwake. Ukioana vayelea?

“Ujue vimeundwa” Lucas alimalizia msemo huo na kushuka kwenye gari.

Aliingiza mabegi ndani na limkuta Juliana akiwa yupo kitandani sura ameikunja. Hakumsemesha alifungua kabati la nguo akaweka hayo mabegi kisha akafunga na funguo kuweka mfukoni. “Noamba nguo zangu niondoke maana naona thamani yangu imeisha alipokuja tu huyo mke wa boss.

“Nguo ameondoka nazo..

“Sasa mimi nitavaa nini?’”

“Sijajua ila fanya uondoke maana atarudi muda si mrefu..

“Kwa hiyo amebeba mpaka chupi yangu”

“Maswali gani sasa hayo ebu fanya uondoke bwana mimi nishachanganyikiwa.”

“Sasa nitaondokaje wewe mwanaume mbona unaongea bila kushirikisha ubongo.

Lucas akafungua kabati akatoa bukta yake na kumpa. Akampa pia na fulana na khanga ya mama Vanesaa. Akafungua waleti na kumpa fedha kama elfu 50 na kumwambia kuwa aende akanunue zingine. Lucas alibadilika na kuwa kama mbogo. Juliana hakuwa ana namna alifanya hivyo na kuondoka zake.Moyoni alikuwa na furaha kuwa pamoja na yote hayo mpango wake wa kubeba mimba yake umefanikiwa.Baada ya kuondoka Lucas alibaki mwenyewe. Aliyafungua yale mabegi ili kuhakikisha kama kweli yalikuwa yamejaa fedha. Ndivyo ilivyokuwa. Alipiga magoti na kumshukuru Mungu. Alijua kabisa kwa bingo hilo ameuaga umasikini.*******

Baba Vanesaa alizikwa na watu walihuzunika sana. Ndugu walifungua kesi kumshtaki mama Vanesaa kwa kumua mumewe ili arithi mali lakni ripoti ya dakari ikamuokoa mwanamke huyo na kifungo. Kesi ilipoisha zilifuata kesi za mirathi. Mama Vanesa tayari alikuwa na ujazito wa Lucas na alitumia ujauzito huo kudanganya kuwa ulikuwa wa marehemu baba Vanesa. Mama Vanesa alishinda kesi na aligawiwa mali nyingi ikiwa ni pamoja na nyumba ya kuishi. Mtoto alipozaliwa hakufanana kabisa na baba Vanesa. Maisha yakawa mtihani mkumbwa sana hivyo aliamua kuachana na familia hiyo. Sasa akawa anaishi na Lucas kama mke na mme. Mtoto aiyezaliwa aliitwa Vanesaa na kufanya mwanamke huyo sasa kustahili jina la mama Vanessa,

Kwa upande wa Juliana mambo yalienda kombo maana licha ya kutarajia kushika mimba siku ile haikuwa hivyo. Mimba haikushika na Llucas hakutoa nafasi ingine tena kwa mwanamke mwingine zaidi ya Mama Vanesaa. Malipo ni hapa hapa duniani maana baada ya kifo cha baba Vanesa majanga makumbwa yalimfika Mishel. Kazi aliyotafutiwa kwa mgongo wa baba Vanesaa alifukuzwa. Maisha yakamwendea kombo na kwa kweli alichangyikiwa sana. Alimtafuta Lucas na kumuomba masahmha lakini alikuwa aechelwa maana Mama Vanesa alikuw ana ujauzitowa pili. Kwa kifupi Mishel alipoteza dira. Maisha yalimpiga fimbo na kumfanya ajute kumsaliti Lucas mwanaume aliyetoka naye mbali.Akadanganyika na mali kwa mara ya pili sasa anawashwa na pilipili ya usaliti. Alikumbuka walipotoka lakini kulikuwa hakuna namna ya kumfanya awe wake tena..Kweli maji yakimwagika hayazoleki. Fedha na utajiri vyote vinapita.. Baada ya muda kupiata mama Vanesa alijifungua mtoto wa kiume. Walimwita Valentine. Kwa sasa wanaishi kwa furaha sana na ni matajiri wakumbwa jijini Mwanza..

************MWISHO*********

JIFUNZE..

Pesa ni matokeo tu ya maisha. Usimsaliti mpenzi wako kisa pesa.. Pesa ni majaliwa usitumie kuwanyanyasa wanyonge na kuwapokonya haki zao.Maisha ni safari jitahidi kusafiri salama.

Comments

Popular posts from this blog

Vifahamu Vitu Vidogo Vidogo Ambavyo Huzidisha Utamu wa Mahusiano Katika Mapenzi

UTAMU WA MCHEZO SEHEMU YA 2

Jinsi ya kumtoa msichana Bikra bila maumivu, wengi hawajui hili, Cheki hapa.