Mpenzi msomaji wangu, katika kuifanya ndoa iwe imara, niliwahi kuzungumzia mavazi sahihi ya mke kumvalia mumewe wakiwa chumbani. Lakini pia nikasema kwamba, kama kwenye nyumba mnaishi wawili tu, sioni shida mke kuvaa anavyotaka. Pia nikasema kuwa, hakuna kitu kibaya kama mke wa mtu kuvaa nguo zisizo za heshima kwenye nyumba ya kupanga kiasi cha kuwatega wapangaji wa kiume. Nilisema hayo baada ya kubaini kuwa, wapo wanawake ambao wameolewa lakini hawaoni hatari kuvaa kimitego bila kujali kuwa, kufanya hivyo ni kuiweka rehani ndoa. Kuna hili vazi la kanga moja ambalo baadhi ya wanawake wamekuwa wakipenda kulivaa hasa maeneo ya mjini, bila kujali ni mchana au usiku, kwenye nyumba ya kupanga au binafsi. Hapo ndipo penye shida na leo nimeona nilizungumzie ili wale wenye tabia hiyo waache mara moja kama wanazitaka ndoa zao. Faida ya Vazi la Khanga Moko Katika Kudumisha Ndoa..... Niseme tu kwamba, ukiwa na mumeo chumbani wala sioni tatizo kumvalia kanga moja, wakubwa wanajua faida ya va...
Dopppp
ReplyDelete