CHOZI LA USALITI[I]

MTUNZI; FRANK DAVID.
"Ama kweli ni bora kukosa pesa sio kukosa furaha maishani" ilikuwa ni siku ya jumapili,siku ambayo baba angu mzazi upenda kutembelewa na wageni, pia ni siku ambayo baba angu utumia kufurahi na familia yake pamoja na wageni na marafiki walio tutembelea.

Lakini siku hiyo nilionekana kuwa mtu mnyonge sana, mpaka baba akanifata na kuniuliza, "mwanangu mbona unaonekana kuwa mnyonge hivyo? Umeshika tama mda wote wenzako tukiwa tunafurahi na kucheka pamoja! Umli wako bado mdogo sana, ndio kwanza miaka 14, napenda kukuona unafuraha sio kuwa mpweke hivyo, Au unaumwa? au una tatizo gani ebu nambie. Nilimjibu na kumwambia "hapana baba siumwi lakini najiuliza sana maswali kichwani mwangu lakini sipati jibu kabisa" baba akacheka! akasema "mhh mwanangu kweli umekuwa kijana mkubwa sasa unafikilia nini hicho ebu niambie"
Siku sita nilimwambia kuwa "Baba umenilea miaka yote vizuri lakini sijawai kumuona mama mzazi mpaka sasa, na kila ninapo muona rafiki yangu Clinton na mama ake natamani sana kuwa na mama pia lakini sina! Baba ebu niambie mama angu yuko wapi Nimuone kidogo tu.Baba alipo sikia tu! aliishiwa nguvu kidogo na akapoteza furaha aliyo kuwa nayo kisha akatokwa na "MACHOZI" akasema mwanangu mama ako ni "MSALITI" sana.

Baba akaendelea na kusema kwamba sikutaka kukwambia mapema lakini kwakuwa umeuliza twende chumbani kwako nikuelezee mama ako mzazi alichofanya; Tuliwaacha wageni wakiburudika ila sisi tukawa chumbani tunaongea tu, Ndipo baba akaniambia mwanangu sio kwamba sikutaka kukulea na mama ako lakini mama ako "tulipendana kipindi tupo chuo, alionyesha upendo mkubwa sana kwangu na heshima! bahati mbaya au nzuri alishika mimba yako tukiwa mwaka wa pili chuo! Alipo niambia kuwa ana mimba yako nilishtuka kwanza maana nilihisi nitamualiabia masomo yake, Na jinsi ya kukulea wewe maana sikuwa na pesa za kutosha wala sikua na kazi zaidi ya pesa za matumizi tena nilizo tumiwa kutoka nyumbani, mama ako alitaka atoe ile mimba, yani wewe sasa! lakini nilimpa moyo na hakutoa mama ako alitoroka kwao kisha akaenda kuishi kwa shangazi yake maana baba ake alikuwa mkali sana hivyo angeweza kumfanya kitu kibaya.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUCHEZEA MATAKO YA MWANAMKE NA KUMPA RAHA YA AJABU KWA KUYABINYA KATIKA MIELEKEO MAALAM SOMA HAPA

UTAMU WA MCHEZO SEHEMU YA 2

MAMA VANESSA SEHEMU YA 16.