Vijue Vyakula Hatari kwa Kupunguza Nguvu za Kiume
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjTeA1Pfkkk2PL4jzVwtNN5ajqUYnIjRPd91n8gGl328v-Eg_HRmEgSYrueA8vUWVYHpyrkdcziMVEvRKVX722fcSmsmzL3cd6IaUdLtRFZslK-pxQMqJE-ldsXfB5Z8gtRrbHbTvlPRno/s400/1.jpg)
Mbegu za Flax (Flax seeds): Wanaume wanapaswa kufahamu aina ya vyakula ambavyo si rafiki kwao katika kuongeza kiwango cha homoni ya kiume iitwayo testosterone inayochochea sifa ya mwanaume yaani kuwa na nguvu za kiume. Baadhi ya vyakula visivyofaa kuliwa na mwanaume aliyetaka kuwa na nguvu za kiume ni vile vyenye asili ya homoni ya kike iitwayo estrogen. Hivyo sio kila vyakula vinafaa kwa mwanaume eti ilimradi tu vyakula hivyo vinasaidia kujenga mwili au kujaza tumbo wakati mtu akiwa na njaa. Vyakula visivyofaa kabisa kuliwa na mwanaume kutokana na vyakula hivyo kupunguza homoni ya testosterone ni hivi vifuatavyo: vyakula vinavyotengenezwa kutokana na unga wa mbegu za flax vimekuwa vikisifiwa kwa kuwa Omega-3 fats ambayo ni muhimu katika miili yetu. Hata hivyo mbegu za flax ni mbegu maarufu kwa kuwa na estrogen ambayo ni sawa kabisa na homoni ya estrogen iliyoko katika miili ya wanawake. Flax seeds zina kiwango cha phytoestrogens mara tatu zaidi ya soya. Kama bado unafikiria kula vya...